
Wizara ya Afya ya Tanzania, Chama cha Ugonjwa wa Kisukari(TDA) na taasisi nyingine muhimu leo Machi 24,wakiwa wameingia katika ushirikiano na Novo Nordisk, wamezindua rasmi mpango wa iCARE.
iCARE™ ni utekelezaji wa mkakati mpya wa uwajibikaji duniani unaoitwa “defeat diabetes (shinda kisukari)” wa Novo Nordisk, barani Afrika.
Lengo la mpango huo ni kuwezesha upatikanaji wa huduma nafuu za kisukari kwa wagonjwa walio hatarini kupata tatizo hilo katika kila nchi na kuhakikisha kuwa hakuna mtoto anayefariki kwa ugonjwa wa kisukari wa aina ya kwanza (diabete 1).

Tanzania ina watu wazima milioni 2.8 (wenye umri kati ya miaka 20 na 79) wanaoishi na ugonjwa wa kisukari na wastani wa uwepo wa ugonjwa huo miongoni mwa watu ni asilimia 10.31.
Wagonjwa wanaoishi na kisukari barani Afrika wanakabiliwa na na changamoto nyingi, hivyo ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi ni muhimu katika kukabiliana na matatizo yenye sura tofauti yanayohusiana na
mapambano ya kuutokomeza ugonjwa wa kisukari.
Mwakilishi wa Serikali ya Tanzania ambaye ni katibu mkuu wa Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi, anakubali kuwa kuna ongezeko la idadi ya wagonjwa wa kisukari barani Afrika na kuna haja ya kuwepo kwa ushirikiano kama huo wa sekta binafsi na umma unaoonyeshwa na mpango wa iCARE™ katika kupambana kwa ufanisi dhidi ya ugonjwa huo na kupunguza mzigo wake, hasa kwa wagonjwa wanaoishi nao, na kwa mapana zaidi katika kusaidia mfumo wa huduma za afya na jamii. Alisisitiza tena nia ya wizara, ambayo tayari ilishathibitishwa kwa barua ya kuunga mkono kuanzishwa kwa mpango huo, kupitia Novo Nordisk.
Mpango wa iCARE™ umezinduliwa rasmi nchini Tanzania ukiwa ni ushirikiano unaohusisha Wizara ya Afya- Tanzania, Chama cha ugonjwa wa Kisukari Tanzania, Umoja wa Magonjwa Yasiyoambukiza (TANCDA), Salama Pharmaceuticals, iMEMS, Christian Social Services Commission(CSSC), Novo Nordisk na ubalozi wa Dernamrk. Mpango huo ni wa miaka mitatu hadi mwaka 2024.
Kitu muhimu katika mkakati wa iCARE™ ni mpango wa unafuu ambao unalenga katika kulinda upatikanaji wa huduma nafuu za kisukari kwa wagonjwa walio hatarini, hasa wa kipato cha chini na walio vijijini ambao hulazimika kusafiri umbali mrefu ili kuweza kupata vitu kama insulin.
Mpango huo unalenga kuwafikia zaidi ya wagonjwa 5,900 kwa kuwawezesha kupata insulin kwa unafuu
katika mikoa tisa, ukifanya kazi katika vituo 75 katika ngazi za wilaya, mikoa na taifa, huku ukijenga uwezo kwa angalau watoa huduma 350 wa afya (HCPs) ifikapo mwaka 2024.