×

Kocha Simba Atoa Tamko la Kibabe Dhidi ya USGN Leo “Hii ni vita ya Kufa au Kupona”

Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco.

ZIKIWA zimebaki saa chache kabla ya Simba haijashuka uwanjani kuvaana na US Gendarmerie katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco, amebainisha kwamba kikosi chake hakina cha kupoteza na kitacheza kufa au kupona kuhakikisha wanatinga robo fainali.

 

Simba leo Jumapili majira ya saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, watashuka Uwanja wa Mkapa, Dar, kuvaana na US Gendarmerie, katika mchezo wao wa sita na wa mwisho wa Kundi D ndani ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Simba inahitaji ushindi wowote kufuzu robo fainali.

Simba walio kwenye nafasi ya tatu na pointi zao saba sawa na RS Berkane walio nafasi ya pili, wataingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kutoa sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya US Gendarmerie uliopigwa nchini Niger, Februari 20, mwaka huu.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Pablo alisema: “Tumefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya mchezo huu, wachezaji wana ari kubwa na wapo tayari kuhakikisha wanatimiza malengo yetu ya kufuzu robo fainali.

 

“Kama ambavyo tumesema hatuwadharau wapinzani wetu licha ya kwamba tutakuwa nyumbani tunajua utakuwa mchezo mgumu.

 

“Lakini tumejiandaa ili kuhakikisha katika mazingira yoyote tunajitoa kila kitu kwa jasho lote kufa au kupona kuhakikisha tunashinda mchezo huu, tunawahitaji mashabiki wetu kuja uwanjani na ni matumaini yetu tutawafurahisha baada ya mchezo.”

SHOLO MWAMBA ASHINDA TUZO 3 kwa MPIGO, AMWAGA MACHOZI NA KUANGUKA STEJINI KWA FURAHA…

Leave a Comment