
TIMU ya SP FC inayomilikiwa na wakazi wa Madale jijini Dar, imecheza mechi ya kirafiki na timu ya Amigos ya Kigamboni, Dar ikiwa ni maandali ya tamasha kubwa la Madale Festival linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Katika mechi hiyo SP FC ya Madale iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wapinzani hao.
Akizungumza na wanahabari Katibu wa maandalizi ya Madale Festival, Revocatus Kahendaguza amesema mechi hiyo ni maadalizi ya tamasha hilo ambalo linatarajiwa kufanyika hivi karibuni.

“Hii ni timu yetu ambayo lengo la kuanzishwa kwake ni kwa ajili ya kutuunganisha wanamadale ili tufahamiane, tushirikiane katika shida na raha pamoja na kepeana fursa mbalimbali.

“Pamoja na kuwa na timu hii tumeamua kufanya tamasha hilo ambalo linarajiwa kushirikisha burudani mbalimbali”, alisema Kahendaguza.
Madale wakitetema baada ya kuichapa Amigos kwa mabao 2-0. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL