×

Tazama Wateja wa NBC Mkoa wa Dar Walivyoandaliwa Iftar

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Theobald Sabi akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla fupi ya Iftar
Baadhi ya wateja wa NBC wa Mkoa wa Dar es Salaam wakipta Iftar katika hafla hiyo.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Theobald Sabi amesema NBC inaendelea kukuza mshikamano na maelewano katika familia na jumuiya kupitia ibada ya iftari.

 

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya Iftar kwa wateja wa NBC wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sabi amesema benki ya NBC imeamua kufanya tukio hili kwa ajili ya kukuza mshikamano na maelewano katika familia na jumuiya.

Baadhi ya wateja wa NBC wa Mkoa wa Dar es Salaam wakipta Iftar katika hafla hiyo.

Sabi amesema, “tunamuni kufunga ni mafunzo, yanaleta maisha ya ukarimu, uchamungu, ukweli, furaha na mshikamano baina ya jamii,”

 

“Tunawashukuru wateja wetu kwa kuitikia wito na kuwa pamoja nasi katika hafla hii muhimu ya Iftar kwa ajili ya kurudisha kwa mwenyezi mungu kupitia ibada ya upendo, kutoa zaka na sadaka,”amesema

Picha ya pamoja 

Aidha, Sabi ameendelea kuhamasisha watu binafsi na taasisi kuendelea kuwasaidia watu wengine kupitia ibada mbalimbali.

Leave a Comment