TAARIFA za kusikitisha zilizoitingisha tasnia ya muziki wa Bongo Fleva usiku wa kuamkia leo ni kifo cha mwanadada Maunda Zorro msanii wa kitambo wa Bongo Fleva ambaye pia ni dada wa msanii mwingine mkongwe wa bongo fleva Banana Zorro
Taarifa za awali zinaeleza kuwa Maunda Zorro amefariki dunia baada ya gari yake kugongana na gari jingine katika eneo la Tuangoma Kigamboni Jijini Dar es salam.
Global TV imezungumza na kaka wa marehemu Banana Zorro ambaye anafafanua zaidi
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amina, kwa taarifa zaidi kuhusiana na taratibu za mazishi endelea kufatilia Global TV online
Enzi za uhai wake, mara kadhaa Maunda Zorro alikuwa akizushiwa kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya jambo ambalo alikuwa akilikanusha vikali na kusisitiza kwamba tuhuma hizo hazina ukweli wowote.
Kupitia kipindi cha mapito alichokifanya Octoba 17, 2021 Maunda Zorro alifafanua kwa kina kuhusu tuhuma hizo na kusisitiza kuwa hatumii na hajawahi kutumia madawa ya kulevya
⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx