Rais Samia Azungumza na Rais wa National Democratic Institute Jijini Washington
Global Publishers April 15, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiwa katika Mazungumzo na Rais wa National Democratic Institute (NDI) Dkt. Derek Mitchell Jijini Washington Nchini Marekani leo tarehe 14 April 2022.
RAIS Samia yupo katika ziara ya kikazi nchini Marekani ambapo amefanikiwa kukutana na viongozi mbalimbali wa kiserikali pamoja na kisiasa, katika moja ya mazungumzo yake amekutana na Rais wa Taasisi ya Demokrasia nchini Marekani Dkt Derek Mitchell iliyopo jijini Washington Marekani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa National Democratic Institute (NDI) Dkt. Derek Mitchell aliyeambatana na ujumbe wake jijini Washington nchini Marekani leo April 14, 2022.