×

Wakala Maarufu Barani Ulaya Mino Raiola Yupo Katika Hali Mbaya

Wakala Maarufu raia wa Italia Mino Raiola

MAPEMA leo zimeibuka taarifa juu ya kifo cha moja kati ya mawakala maarufu wa wachezaji barani Ulaya Mino Raiola ambapo vyombo mbalimbali vya habari duniani vimeripoti kifo chake kabla ya kukanusha taarifa hizo.

 

Katika hali ambayo imewaacha na mshangao mkubwa mashabiki na wadau wa soka duniani kote ni kwamba Wakala huyo ambaye taarifa za kifo chake zimeenea duniani kote ametoa taarifa kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Twitter akiandika:

Mino Raiola aliyekuwa wakala wa Erling Haaland, Paul Pogba na Zlatan Ibrahimovic

“Hali ya sasa ya afya kwa mtu anayedhaniwa, ni kwa mara ya nne sasa ndani ya miezi kadhaa wameniua. Inaonekana pia naweza kuzinduka.”

 

Mino Raiola ni moja ya mawakala wakubwa ambaye anawasimamia wachezaji mastaa wakubwa duniani akiwemo Erling Haaland, Paul Pogba pamoja na Zlatan Ibrahimovic.

 

 

Leave a Comment