×

Makamu wa Rais Awasili Kigoma Kuhudhuria Msiba ya Askofu Katale

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma akisalimiana na Mkuu wa Mkoa huo Mheshimiwa Thobias Andengenye wakati alipowasili mkoani Kigoma kushiriki mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Ziwa Tanganyika la Kanisa la Morovian,Askofu Charles Katale yanayofanyika leo tarehe 7 Mei 2022.

MAKAMU WA RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, Philip Mpango amewasili mkoani Kigoma kwa ajili ya kuhudhuria msiba wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Ziwa Tanganyika Charles Katale aliyefariki ghafla Mei 2 mwaka huu.

 

Askofu Katale alifariki wakati uongozi wa Jimbo hilo ambao Makao Makuu yake yapo mkoani Kigoma ukiwa katika harakati za kumsafirisha kumpeleka mkoani Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi.

Makamu wa Rais baada ya kutua na Ndege mkoani Kigoma akielekea kwenye msiba wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Moravian Tanzania Charles Katale

Taarifa ya kifo chake ilitolewa na Askofu Kiongozi wa Kanisa la Moravian Tanzania, Conrad Sikombe.

 

Baada ya Kifo chake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alituma salamu za pole na kuoneshwa kusikitishwa na kifo cha Askofu Charles Katale.

Leave a Comment