RAPA na mwanamitindo maarufu duniani, Kanye West (38) juzi Jumanne alitajwa kuwa GQ Most Stylish Man of 2015 kwa mara ya pili mfululizo.
Kanye (kulia), mkewe Kim Kardashian na mtoto wao North West.
Hii imekuja baada ya kupata kura nyingi zaidi kuliko washindani wake, kura alizozipata kwa ‘sapoti’ kubwa kutoka kwa mkewe, Kim Kardashian na dada zake Kim (Khloe na Kourtney) pamoja na mama yao Kris Jeaner kuwashawishi mamilioni ya mashabiki wao mitandaoni wampigie kura Kanye ili ashinde.
Mastaa aliyokuwa akichuana nao.
Taarifa ya GQ zinasema, Kanye alishinda kwa kupata kura 520,119 wakati mpinzani wake ‘modo’ Lucky Blue Smith mwenye umri wa miaka 17 akimaliza kwa kupata kura 445,073.
Kanye alikuwa akishindana na mastaa 64 wakiwemo mcheza soka maarufu Mario Balotelli, mwana-hip-hop, Jay-Z, Lewis Hamilton na staa wa Game Of Thrones, Kit Harington.
Kwenye fainali, Kanye aliwashinda mwigizaji maarufu wa filamu na mwanamuziki Jared Leto, Lucky na Robbie Roggers.
Staili mpya ya viatu aina ya ‘Yeezy Boosts’ vya Kanye
GQ wameongeza kuwa, staili ya mwaka ya viatu vya Kanye inayojulikana kama Yeezy akishirikiana na Kampuni ya Adidas, staili iliyozinduliwa February kwenye New York Fashion Week ndiyo imembeba zaidi Kanye.
Baada ya ushindi huo, Kanye West aliandika hivi “Thank you GQ and to everyone who voted, it’s been an amazing year!!!”.


