×

Kibwana Shomari Asaini Miaka 2 Kuendelea Kuwatumikia Wanajangwani

Beki wa Yanga Kibwana Shomari akiwa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo Dkt, Mshindo Msolla

BEKI wa Kulia wa Klabu ya Yanga Kibwana Shomari amesaini mkataba wa miaka mwili kuendelea kuitumikia timu ya wananchi Yanga.

Mkataba wa Kibwana ulikuwa unamalizika mwisho wa msimu huu, hivyo kwa mkataba huo ataendelea kuwatumikia wananchi kwa miaka mingine miwili mbele.

Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya Yanga Injinia Hersi Said kutoka GSM akiwa na Mlinzi wa Klabu ya Yanga Kibwana Shomari

Taarifa za kuongezwa kwa kandarasi ya Kibwana Shomari zimethibitishwa na Klabu ya Yanga kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

Leave a Comment