Liverpool Yatwaa Ubingwa wa FA, Yaichapa Chelsea kwa Mikwaju ya Penati
KLABU ya Liverpool imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Kombe la Shirikisho nchini Uingereza maarufu kama FA baada ya kuichapa klabu ya Chelsea kwa mikwaju ya penati 6-5
Mchezo ulimalizika kwa matokeo ya bila kufungana kwa dakika 90 kabla ya kuongezwa dakika nyingine 30 ambapo nazo zilimalizika kwa timu hizo kutofungana ndipo ikafuata changamoto ya mikwau ya penati ambapo Liverpool walifanikiwa kufunga penati 6 na Chelsea kufunga penati 5
Waliokosa penati kwa upande wa Chelsea ni Cesar Azpilicueta na Mason Mount huku Sadio Mane akikosa mkwaju wa penati kwa upande wa Liverpool
Kwa ushindi huo Liverpool inakuwa imefanikiwa kutwaa makombe mawili ya ndani kwa maana ya kombe la Carabao pamoja na Kombe la FA na yote yakiwa yamechukuliwa kutoka kwa Chelsea kwa njia ya mikwaju ya penati.