
Klabu ya Simba imefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho Azam Sports baada ya kuitandika Pamba FC kwa jumla ya mambao 4-0.

Mabao ya Simba yaliwekwa kimiani na Peter Banda katika dakika ya 45, Kibu Denis katika dakika ya 48 na Yusuph Mhilu aliyefunga mabao mawili katika dakika za 53 na 89.
Kwa matokeo hayo klabu ya Simba itakutana na mahasimu wao Yanga katika pambano la nusu fainali ya kombe hilo huku