
MSANII wa kitambo wa Taarab, Aisha Vuvuzela amesema kuvunjika kwa Bendi ya Taarab ya Ya TMK kumemfaidisha kwa sababu baada ya kuachana na bendi hiyo, alipata akili za kufungua bendi yake anayoendelea nayo hadi leo.
Akifanya mahojiano na @255globalradio na Global TV, amesema kuwa kipindi akiwa nyumbani baada ya bendi kuvunjika, ndipo alipopata wazo la kujaribu kuanzisha bendi yake na alipofanya hivyo, alishangaa jinsi alivyopokelewa na mashabiki wake.
Akizungumzia changamoto ambazo amekuwa akikutana nazo katika kuisimamia bendi yake, amesema wasanii wanapohama kutoka bendi yake kwenda nyingine, huwa inamvuruga lakini ameshajua namna ya kukabiliana na changamoto hiyo na anaendelea vizuri.