
MKURUGENZI MKUU wa Program ya Kudhibiti na kuzuia magonjwa Amref Health Africa Tanzania Dkt.Rita Mutayoba amesema kuwa Tanzania kwa ufadhili wa Africa CDC kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Ofisi ya Rais TAMISEMI na Kamati za Afya Mikoa ya Simiyu na Tanga katika kutekeleza mradi wa chanjo ya UVIKO-19 unaolenga kuharakisha upatikanaji wa chanjo kwa wananchi katika Mikoa ya hiyo Amref inatoa elimu na kuhamasisha jamii kutumia chanjo ya UVIKO-19 kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutumia mitandao ya jamii ambapo matarajio yetu ni kufikia wananchi wengi iwezekanavyo na taarifa sahihi kuhusu chanjo ya UVIKO-19 na kuongeza mwamko wa wananchi kutumia chanjo hii.
Katika kuendeleza jitihada za Serikali mwaka huu Shirika la Amref Health Africa Tanzania limeamua kufanya kampeni ambayo itachangia katika kusambaza elimu na hivyo kutoa hamasa kwa wananchi kupata chanjo ya UVIKO 19 huku lengo kuu likiwa kuisaidia serikali kufikia lengo la asilimia 70 ya watu wote wanaostahili kuchanja ifikapo Desemba mwaka huu.
“Kampeni hii inalenga kupeleka elimu kwa watanzania wote ambao wanastahili kupata chanjo kundi hili ni la watanzania wote wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea”.
Kampeni hii inahusisha pia wahamasishaji wa mitandaoni ambao wamekuwa na ushawishi mkubwa katika masuala mbalimbali ya jamii.

Wahamasishaji hawa hutumia kurasa zao mitandaoni kwa kuweka taarifa sahihi juu ya chanjo pamoja na UVIKO 19.
Taarifa hizi hupitiwa na Wizara ya Afya kabla ya kuwekwa mitandaoni zimekuwa msaada mkubwa kwa wale wanaozipokea.