×

DC Gondwe Asisitiza Usafi Kinondoni ni Kila Siku na Ada ya Usafi ni kwa Kila Familia

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe ameongoza kwa mfano katika zoezi la usafi lililofanika maeneo ya Kata ya Wazo, Tegeta Magereji Jijini Dar es Salaam.

 

Katika zoezi hilo Gondwe amewaasa wananchi kuendelea kutekeleza kwa vitendo zoezi la usafi wa mazingira kila siku kwa hiari ikiwemo mazingira ya nyumba zao, Ofisi zao lakini pia miundombinu kama vile mitaro kwani yote hiyo ni mali yao na si ya Serikali.

 

Gondwe amesisitiza kuwa maelekezo kuhusu ada ya usafi ni kwa kila familia hata kama kwenye kaya moja kuna familia tano basi kila familia itatakiwa kutoa mchango wa usafi na hilo ni suala mtambuka ambalo linahitaji utekelezaji.

DC Gondwe amebainisha kuwa usafi ndani ya Wilaya ya Kinondoni ni kila siku

Mkuu huyo wa Wilaya amebainisha kuwa wao kama Serikali wanajukumu moja tu kubwa la kuhakikisha magari yanayohusika na kubeba takataka yanakuja kwa wakati na pale inapotokea kuna uchelewaji wa namna yoyote ile basi mamlaka za serikali za mtaa na ngazi nyingine za uongozi zipewe taarifa kwa ajili ya hatua zaidi.

Leave a Comment