Barua ya Rais Samia Yasomwa Bungeni, Ni Kuhusu Tuzo ya Babacar Ndiaye

RAIS Samia Suluhu Hassan, ameliandikia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, barua ya salamu za shukrani kuwashukuru wabunge kwa kujadili na kutoa azimio la kumpongeza baada ya kupata tuzo ya Babacar Ndiaye nchini Ghana, ambayo hupatiwa Rais wa nchi za Afrika zinazofanya vizuri kwenye miundombinu ya barabara.
Barua hiyo imesomwa leo Jumatatu, Mei 30, 2022, na Spika wa Bunge hilo, Dkt. Tulia Ackson.

“Kwa kipekee kabisa tuzo hiyo ni ya wabunge kwa kutambua mchango wenu katika kusimamia miradi, matumizi sahihi ya fedha za miradi na kupitisha na kusimamia bajeti ya serikali hivyo ninaomba Watanzania wote wafurahie tuzo huku tukiendelea kusimamia, kulinda na kuitunza miundombinu yetu,” imeeleza sehemu ya barua ya Rais Samia kwa Bunge.