Mgombea-mwenza wa kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akihutubia wanachama wa CCM na wananchi Jimbo la Madaba katika Kijiji cha Mtyangimbole na Limbuka kwenye mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Wilaya wa Limbuka, mkoani Ruvuma leo Septemba 15, 2020.
Wanachama wa CCM na wananchi wa Madaba wakimsikiliza Samia Suluhu. Samia Suluhu, akizungumza katika mkutano huo.