
WAZIRI MKUU wa Uingereza Boris Johnson anatarajiwa kupigiwa kura ya kukosa Imani na wabunge wa Chama chake cha Conservative.
Hali hiyo imeibuka baada ya kuwa na mijadala mingi ya kumtaka Waziri huyo kujiuzuru baada ya kukumbwa na kashfa nyingi ikiwemo ile ya kuandaa tafrija wakati wa katazo la kuandaa matukio ya sherehe na hafla mbalimbali nchini Uingereza kutokana na maambukizi ya virusi vya Uviko -19.

Katika tukio hilo Waziri Mkuu Johnson alikuwa miongoni mwa waliolimwa faini na Polisi wa eneo la Downing Street kutokana na kukiuka sheria za kupambana na maambukizi ya virusi vya Uviko-19.
Siku ya Leo Waziri Mkuu huyo endapo atapigiwa kura nyingi za kukosa Imani basi atalazimika kujiuzuru wadhifa wake huo.
Boris Johnson aliingia madarakani mwaka 2019 akirithi mikoba ya Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo Theresa May.