×

Senzo: Kwa Kipindi cha Miezi 6 Tumekusanya Bilioni Moja za Kitanzania -Video

Senzo Mbatha Mazingiza CEO wa Yanga

MKURUGENZI Mtendaji wa Klabu ya Yanga Senzo Mbatha Mazingiza amesema kupitia mfumo wa kidigitali wa mabadiliko ya Klabu ya Yanga ulioasisiwa mapema mwaka huu klabu hiyo imeingiza zaidi ya Bilioni moja za kitanzania.

 

Senzo amebainisha kuwa kwa msimu wa mwaka 2019 Yanga ilikusanya zaidi ya kiasi cha milioni 9 kupitia pesa za usajili wa wanachama, msimu wa 2020 Yanga ilikusanya kiasi cha milioni 6.5 na msimu uliopita Yanga ilikusanya Zaidi ya milioni 21 kupitia usajili wa wanachama.

Yanga imekusanya zaidi ya Bilioni moja tangu mchakato wa mabadiliko uanze

“Kwenye kikao chetu na Makamu Mwenyekiti alisema watu hawawezi kuamini kama tukiwaambia kuhusu namba hizi lakini tumekusanya Zaidi ya bilioni moja kwa kipindi cha miezi sita tu.” Alisema Senzo akiongea na waandishi wa habari.

 

Kwa upande mwingine Senzo amewashukuru wadau wa Yanga Kampuni ya Kili net kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha zoezi hilo kwenda vizuri kwa kipindi cha miezi sita tangu mradi ulipoanza.

Leave a Comment