×

RC Mbughe Amshukuru Rais Samia kwa Kupeleka Bilioni 351 Mkoani Kagera

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbughe

MKUU wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbughe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka kiasi cha shilingi Bilioni 351 mkoani humo ambazo ni fedha za maendeleo kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi Februari 2022.

 

RC Mbughe ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT amemsifia Rais Samia kwa ubunifu wake katika uandaaji wa Filamu ya The Royal Tour ambayo kimsingi hadi sasa umechangia kuvutia idadi kubwa ya watalii nchini.

Wananchi Wilayani Biharamuro wakimsikiliza Rais Samia

RC Jenerali Mbughe amesema kwa upande wa madarasa Mkoa wa Kagera umefanikiwa kujenga idadi ya madarasa 881 ambapo katika Wilaya ya Biharamuro pekeyake yamejengwa madarasa 159 na kuhakikisha hakuna Shule ambayo imekosa madarasa.

Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa Biharamuro mkoani Kagera

Akitoa ripoti kwa Rais Samia kuhusu hali ya Uviko-19 ndani ya Mkoa huo Meja Jenerali Mbughe amesema Elimu inaendelea kutolewa kwa wananchi kuhusu kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo lakini kubwa zaidi ni kwamba wananchi wanaendelea kupata chanjo kama kawaida.

Leave a Comment