×

Urusi: Ukraine Imepata Hasara Kubwa huko Donbas Yapoteza Wanajeshi 300, Mizinga 3

 

Ukraine inakabiliwa na hasara kubwa miongoni mwa wanajeshi wake , silaha na zana za kijeshi katika eneo la mashariki la Donbas, Urusi imesema katika akaunti yake hivi punde kuhusu vita.

Wizara yake ya ulinzi ya Urusi inadai Ukraine ilipoteza zaidi ya wanajeshi 300, mizinga sita na magari wakati wa siku tatu za mapambano katika mji wa Svyatogorsk.

Mashambulizi ya mizinga katika eneo la Zaporizhzhia yamesababisha vifo vya wananchi wengine 320 wa Ukraine.

Ndege mbili zaidi za Ukraine na helikopta zimedunguliwa katika eneo la Mykolaiv

Makombora ya hali ya juu yamelenga shabaha ikiwa ni pamoja na viwanda na ghala la silaha ndani na karibu na mji wa Kharkiv, kaskazini.

Urusi imejaribu kuhalalisha uvamizi wake kwa misingi kwamba inawaondoa raia wa Ukraine kutoka kwa madai ambayo yanaonekana na Kyiv na ulimwengu wa nje kama propaganda zisizo na msingi.

Leave a Comment