DCB Yasherehekea Miaka 20 Ya Mafanikio kwa Kutoa Fursa za Kiuchumi
Global Publishers June 14, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB, Zawadia Nanyaro ( kushoto ) akipokea tuzo ya shukrani ya Hayati Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya huduma bora ya benki hiyo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Uanzishwaji wa DCB ilikuwa moja ya ndoto za hayati Mkapa katika kuwasaidia wafanyabiashara ndogondogo waliokosa vigezo vya kupata mikopo ya mitaji kupitia mifumo rasmi ya kibenki. Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omar Kumbilamoto ( kulia ) akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB, Pamela Nchimbi wakati wa sherehe ya Maadhimisho ya miaka 20 ya mafanikio ya benki hiyo yaliyofanyika jijini leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Hanifa Suleiman Hamza na Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa.Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB, Zawadia Nanyaro ( katikati ), aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kwanza wa benki hiyo, Edmund Mkwawa ( kulia ), Katibu Muhtasi wa benki hiyo, Judith Maeda, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa, Mhasibu wa Tawi wa benki hiyo, Prisca Dona, Ofisa Rasilimali Watu wa benki hiyo, Rosemary Masaga na Mwenyekiti wa Bodi Mstaafu wa benki hiyo, Prof. Lucian Msambichaka wakipiga picha ya kumbukumbu …Zawadia Nanyaro ( katikati ) akikabidhi tuzo ya shukrani kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kwanza wa benki hiyo, Edmund Mkwawa wakati wa sherehe ya Maadhimisho ya miaka 20 ya mafanikio ya benki hiyo