
KIONGOZI Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ameipongeza nchi ya Ukraine kwa kupambana kutetea uhai wao dhidi ya uvamizi wa Urusi.
Katika toleo lililochapishwa na jarida la Catholic siku ya jumanne limeeleza kuwa Papa Francis amebaini kuwa vita hiyo ingeweza kuzuiliwa mapema kama pande zote mbili zingeona umuhimu wa kuzuia vita hiyo.

Papa Francis amelaani kitendo cha Urusi kuivamia Ukraine akidai kuwa wanajeshi wake wamefanya ukatili, mauaji na vitisho dhidi ya watu ambao wanapambania uhai wao.
Kiongozi huyo mkubwa wa dini ya Katoliki Duniani amehusisha vita hiyo na biashara ya zana za kivita kama kichocheo mkikubwa cha kuendelea kwa vita hiyo.
“Ni wazi kwamba Urusi wao waliamini vita hii ingeweza kutamatika ndani ya wiki moja, lakini walipiga hesabu zao vibaya. Walikutana na watu madhubuti ambao wanapambana kwa jasho na damu kutetea uhuru wao na ambao wana historia ya mapambano.” Aliongea hayo kupitia jarida la Civilta Cattolica.

Papa Francis akiongea na mhariri wa jarida la Jesuit alibainisha kuwa mwezi mmoja kabla ya Putin kutuma vikosi vyake kwa mara ya kwanza kuvamia ardhi ya Ukraine alibainisha kuwa NATO walikuwa wakibweka nje ya mlango wa Urusi ndiyo maana hakuwa na namna nyingine zaidi ya kuanza mashambulizi.
Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Putin na kama anaunga mkono kile kinachoitwa Operesheni ya kuwaondoa watu wenye dhana ya mlengo wa kinazi katika nchi ya Ukraine Papa Francis aligoma akidai kuwa itakuwa ni kitu cha kushangaza sana kama mtu ataunga mkono jambo hilo.