
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua Profesa Eliamani Sedoyeka kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, awali Profesa Sedoyeka alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Kwa upande mwingine Dk Francis Michael yeye ameteuliwa kuchukua nafasi ya Profesa Sedoyeka katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus ni kwamba tarehe rasmi ya kuapishwa kwao itatangazwa baadae.
