×

Ukraine Yakaribia Kujiunga na Umoja wa Ulaya EU, Rais Abariki

Rais wa Umoja wa Ulaya EU, Ursula von der Leyen

Nchi ya Ukraine imepiga hatua nzuri katika jitihada zake za kujiunga na Umoja wan chi za Ulaya EU, hayo yamebainishwa na Rais wa Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen.

 

Rais huyo amesema Ukraine kwa sasa instahili kupewa hadhi ya Ugombea lakini ili kupata kibali rasmi cha kujiunga na Umoja wa Ulaya nchi hiyo inalazimika kufanya mabadiliko muhimu ikiwemo utawala wa demokrasia, marekebisho kwenye sheria za haki za binadamu pamoja na mifumo ya kuzuia na kupambana na rushwa.

Idadi kubwa ya wanajeshi nchini Ukraine wamefariki kutokana na vita hiyo

Hadhi ya Ugombea hupewa nchi kabla ya kujiunga rasmi ingawa hatua hiyo inaweza kuchukua miaka mingi hadi Ukraine iweze kuthibitishwa kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

 

Akiongea kutokea Brussels nchini Ubelgiji huku akiwa amevalia mavazi ya njano na bluu ambazo ni rangi za Ukraine, Von der Leyen amesema raia wa Ukraine walikuwa tayari kufa kwa ajili ya nchi yao.

 

“Tunataka nao waishi kama sisi kwenye ndoto ya pamoja ya mataifa ya Ulaya, Ukraine wameonesha nia na haja ya kuishi kwa kuzingatia miiko pamoja na hadhi ya umoja wa Ulaya lakini kuna vigezo vyake ambavyo Ukarine lazima ifuate ili sheria za kimataifa ziweze kufuatwa na kuheshimiwa.” Alisema von der Leyen.

 

 

 

Leave a Comment