×

Picha Mpya za 2pac Zawa Gumzo, Mashabiki Wadai Anaweza Kuwa Hai

2pac Shakur

ALIYEKUWA rapa kutokea Marekani, 2pac Amaru Shakur aliyefariki mwaka 1996, amezua gumzo na taharuki katika mitandao mbalimbali ya kijamii baada ya picha zake mpya kusambaa.

 

Watu wengi wamehoji iwezekanaje picha za rapa huyo aliyefariki miaka 26 iliyopita, kuonekana na ubora zaidi kushinda hata baadhi ya picha za watu mbalimbali ambao bado wapo hai.

 

 

Tupac amefariki mwaka 1996

“Picha za Tupac zina ubora kuliko picha za baadhi yetu tulio hai,” aliandika shabiki moja.

 

“Tupac alikuwa na iphone 13 mwaka 1995?” aliuliza shabiki mwingine.

 

Utata huo umefanya baadhi ya watu kuamini kuwa inawezekana, Tupac bado yupo hai kutokana na utata wa kifo chake, huku wengine wakimtaka rapa huyo kujitokeza kama bado yupo hai.

2pac anadaiwa anawezqa kuwa hai

“Tunajua bado upo hai Pac, tafadhali jitokeze tumekukumbuka sana.” aliandika shabiki mwingine.

Leave a Comment