×

RC Mwanza Aagiza Takukuru Kuchunguza Upotevu wa Milioni 15 Buchosa

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Robert Gabliery

MKUU wa Mkoa wa Mwanza Robert Gabliery ameagiza Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) kuchunguza upotevu wa takribani kiasi cha shilingi milioni 15 ambazo ni fedha za Maendeleo kwenye Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema Mkoani humo.

 

Hili limesababishwa na kiasi cha shilingi milioni 15 kuonekana kuwa zilihamishwa kutoka katika akaunti ya mapato ya ndani na kwenda kwenye akaunti ya maendeleo ya Halmashauri lakini katika hali ya kushangaza ni kwamba pesa hizo hazijaonesha kupokelewa katika akaunti husika.

Madiwani wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza

Kufuatia sakata hilo Mkuu wa Mkoa ametoa kauli hiyo kwenye kikao maalumu cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Buchosa cha kujadili hoja za Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).

 

Halmashauri ya Buchosa ni miongoni mwa Halmashauri nane zinazounda Mkoa wa Mwanza, ambapo tangu ianzishwe mwaka 2015 imekuwa na mwenendo wa kupata hati safi licha la kupata hati ya mashaka kwa miaka miwili ya 2016/17 na 2018/19.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ameagiza Takukuru wafanye kazi ya kuchunguza upotevu huo wa shilingi milioni 15

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga ameahidi kufuatia suala hilo na baada ya ukweli kufahamika juu ya sakata hilo basi hatua za kisheria zitachukuliwa juu ya wahusika.

 

 

Leave a Comment