×

Boris Johnson: Kama Putin Angekuwa Mwanamke Naamini Asingevamia Ukraine

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson

WAZIRI MKUU wa Uingereza Boris Johnson ameibuka na kusema kuwa kama Rais wa Urusi Vladimir Putin angekuwa mwanamke basi asingeweza kuvamia nchi ya Ukraine.

 

Johnson ameyasema hayo huku akitoa rai kwa jumuiya za kimataifa na mataifa mbalimbali kuongeza jitihada katika kuhakikisha viongozi wengi wanawake wanapata fursa katika nyadhifa za juu za uongozi.

 

“Kama Putin angekuwa mwanamke, na ni kitu ambacho naamini kabisa siyo lakini najaribu kufikiria tu kama angekuwa mwanamke naamini asingefanya alichofanya cha kuvamia nchi ya Ukraine, na ndiyo maana kuna kila sababu ya kuweka jitihada kuhakikisha tunakuwa na idadi kubwa ya wanawake katika nafasi zenye nguvu na maamuzi.” alisema Johnson.

 

Waziri Mkuu huyo ameongea maneno hayo kuelekea mkutano wa Jumuiya ya Umoja wa Kujihami wan chi za Ulaya (NATO) ambao unatarajiwa kujadiliana kuhusu hatua madhubuti za kuchukua dhidi ya vitisho vinavyoendelea vya serikali ya Urusi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin

Mataifa yote washirika wa NATO wamekubaliana kuchangia asilimia 2 ya pato lao la ndani kama sehemu ya bajeti ya kuimarisha usalama kwa nchi wanachama, ingawa hadi kufikia mwaka 2021 lengo lilikuwa limefikiwa au kuzidi na nan chi 8 wanachama ikiwemo Marekani.

 

Katibu wa Wizara ya Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace amemshauri Waziri Mkuu Johnson kuongeza matumizi katika ununuzi wa zana za kivita ili kujilinda na vitisho vinavyosababishwa na nchi ya Urusi.

Leave a Comment