
KIUNGO wa klabu ya Yanga Salum Abubakar SureBoy huenda lewo akatengeneza historia ya kipekee kwa wachezaji wa kitanzania kama klabu yake ya Yanga itaibuka na ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar katika pambano la mwisho la Ligi Kuu ya NBC linalotarajiwa kupigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa kumi kamili jioni.
Mchezaji huyo ambaye kwenye mchezo wa leo dhidi ya Mtibwa Sugar hajapangwa ataweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee wa kitanzania kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu bilakupoteza mchezo hata mmoja akiwa na klabu mbili tofauti ya Azam na Yanga.

SureBoy alisajiliwa na Yanga akitokea klabu ya Azam katika dirisha dogo la mwezi Januari huku akiwa na mchango mkubwa katika kuisaidia klabu yake ya Yanga kuibuka na mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu.
SureBoy alichukua ubingwa wa kwanza akiwa na klabu ya Azam mwaka 2014, akichukua bila kupoteza mchezo hata mmoja ambapo mwaka huu pia anatarajiwa kuchukua ubingwa wake wa pili kama Yanga itafanikiwa kutopoteza mchezo wake dhidi ya Mtibwa Sugar.