
KIKUNDI cha waandamanaji katika Mji Mkuu wa Libya, Tripoli wamepiga mawe Jengo la Bunge ikiwa ni sambamba na kuchoma moto matairi kama ishara ya kushinikiza mabadiliko ya uongozi ndani ya nchi hiyo ambayo yanaambatana na mabadiliko ya katiba ya nchi.
Taarifa zinadai sehemu ya Jengo hilo la Bunge liliwashwa moto na waandamanaji waliopo Mashariki mwa Mji wa Tobruk.
Katikati ya mji waandamanaji wamepaza sauti zao kudai kugfanyika kwa uchaguzi mkuu.
Madai yao yameungwa mkono na kiongozi wa serikali ya muda Hamid Dbeibah aliyesema Katiba ya nzima ya nchi hiyo inahitaji mabadiliko.

Maandamano hayo yameibuka mara baada ya Umoja wa Mataifa jijini Geneva Uswisi kusitisha kile kinachosadikika kuwa ni hatua muhimu katika mazungumzo ya kutengeneza njia ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Libya.
Libya imekuwa kwenye machafuko tangu kuondolewa madarakani kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011 baada ya vita iliyoratibiwa na vikosi vya NATO kumuua kiongozi huyo.