×

Kenya: Asilimia 80 ya Shisha ina Coacaine

shisha

Wizara ya Afya imesema asilimia 80 ya Shisha inayovutwa nchini humo ina chembechembe za Madawa ya Kulevya aina ya Cocaine.

Waziri wa Afya nchini humo aliyasema hayo jana ikiwa ni Siku ya Kupinga Matumizi ya Tumbaku Duniani kama ilivyoainishwa kwenye kalenda ya Shirika la Afya Dunani (WHO) ili kuwatahadharishana kuwaelewesha umma hususani kuhusu madhara mabaya kwa afya ya binadamu yatokanayo na matumizi ya tumbaku na sigara kwa ujumla ikiwemo kupinga matumizi hayo.

Waziri aliandika kwenye mtandao wa Twitter kuwa, wamegundua kuwemo kwa chembechembe za madawa ya kulevya aina ya cocaine yaliyokuwa kwenye shisha nne kati ya tano walizozifanyia uchunguzi.

“Tumefanya utafiti kwenye shisha zaidi ya 300 na kugundua kuwa asilimia 80 ya shisha zinazovuta Kenya zin amadfawa ya kulevya yakiwemo cocaine,” Nacada Chairman Mututho, alisema.

Leave a Comment