Breaking: Matokeo ya Kidato cha Sita na Ualimu Yatangazwa, Yatazame Hapa

BARAZA la Mitihani la Tanzania leo tarehe 5/07/2022 limetangaza matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Sita na Ualimu 2022. Matokeo hayo yanapatikana kwenye tovuti ya NECTA.
Matokeo hayo yametangazwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Athuman Salum Almasi. Almasi amezitaja shule zilizoingia kumi bora kwa ufaulu kuwa ni kama ifuatavyo:
1. Kemebos- Kagera
2. Kisimiri- Arusha
3. Tabora Boys- Tabora
4. Tabora Girls- Tabora
5. Ahmes- Pwani
6. Dareda- Manyara
7. Nyaishozi- Kagera
8. Mzumbe- Morogoro
9. Mkindi- Tanga
10. Mziba- Tabora.
YASOME HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA
Pia tazama Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athuman Salum Almasi akitangaza matokeo hayo.

