×

Anunua Ice Cream ya Kopo na Kukuta Chura Ameganda, Adai Imetoka Kama Ilivyo Kiwandani

Ice cream aina ya Blue Bunny

MWANAMKE mmoja aliyefahamika kwa jina la Tracy Wiemelt Holtman yamemkuta baada ya kununua Ice cream dukani lakini alipofungua bakuli husika ndio akakutana na mauzauza hayo chura huyo akiwa ameganda kwenye Ice cream.

 

Amesema inavyoonekana hata duka husika nao walipewa hivyo toka kiwandani kwani Ice cream ilikuwa imefungwa vizuri haikuonesha kufunguliwa.

 

Amesema atairudisha duka husika aliponunua ingawa anahisi wanaweza wasimuamini kuhusu chura hilo lililoganda kwenye Ice cream hiyo.

 

Mrembo huyo alitumia ukurasa wake wa Facebook kuchapisha picha hiyo na kueleza alivyomkuta chura mkubwa kwenye Ice Cream yake hiyo aina ya Blue Bunny.

Leave a Comment