×

Msafara wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari Washambuliwa kwa Risasi

                       Msafara wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari

WATU  wenye silaha wameshambulia msafara wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari huko Katsina, jimbo anakotoka kaskazini mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa Rais Garba Shehu amesema watu wawili walipata majeraha katika msafara wa awali wa walinzi

Msafara huo ulikuwa umeenda kabla ya safari ya Rais kuelekea mji wake wa Daura kusherehekea sikukuu ya Eid-ul-Adha ya Waislamu wikendi hii wakati washambuliaji walipowafyatulia risasi.

Hata hivyo jeshi lilifanya mashambulizi ya kujibu na kuwazuia na shambulizi lao ofisi ya Rais ilisema Katsina ni mojawapo ya majimbo ya kaskazini-magharibi mwa Nigeria yaliyoathiriwa na vitendo vya uhalifu wa majambazi .

 

Leave a Comment