The House of Favourite Newspapers

Travis akana kuzuia albamu ya Rihanna

0

2D217D6B00000578-3261931-image-a-19_1444143891453Rihanna.

LOS ANGELES, Marekani

MSANII classic, Rihanna yupo kwenye msukumo mkubwa kutoka kwa mashabiki wake ambao wanataka kuona anatoa albamu yake ya ANTI ambayo imekuwa ikipigwa kalenda lakini imedaiwa kuwa mpenzi wake, Travis Scott ndiye amekuwa chanzo.

Imeripotiwa kuwa awali albamu hiyo ilikuwa itoke Novemba 6, mwaka jana, ikasogezwa mbele hadi sikukuu ya Krismasi lakini pia ikashindikana na mpaka sasa ipo kabatini mwake na ikumbukwe mara ya mwisho kwa msanii huyo kuachia albamu ni mwaka 2012.

rs_634x1024-150911083520-634-2rihanna-edition-nyfw-travis-scott.ls.91115Rihanna akiwa na mpenzi wake Travis Scott.

Mwandishi anayemuandikia pia ngoma Rihanna ambaye pia ni prodyuza, John Glass amesema aliyesababisha albamu hiyo kuchelewa ni Travis na kwamba awali walikubaliana vizuri na Rihanna na akautangazia ulimwengu kuwa kuna kazi inakuja lakini Travis alionekana kama kuweka ‘dauti’ kwenye hilo huku akidaiwa kumpa ushauri mbaya RiRi.

Hata hivyo kuonyesha kuwa hahusiki na suala hilo Travis amejibu kwa kudai kuwa hakuna kitu kama hicho.

Leave A Reply