×

Putin Kukutana na Rais wa Iran na Uturuki Kujadili Mustakabali wa Syria na Ukraine

Rais wa Urusi Vladimir Putin

RAIS wa Urusi Vladimir Putin anatarajiwa kukutana na rais wa Iran Ebrahim Raisi huko Tehran katika kikao ambacho pia kitamhusisha Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

 

Imeripotiwa kuwa lengo kuu la kikao hicho ni kutafuta suluhu juu ya mgogoro unaoendelea nchini Syria lakini pia kutatua changamoto ya uhaba wa chakula nchini Ukraine.

Rais Putin anatarajiwa kuongea na Rais wa Iran Ebrahim Raisi pamoja na Rais wa Uturuki Recep Erdogan

Kumekuwa Na mgogoro uliodumunkwa muda mrefu kati ya Uturuki na Syria ambapo Utruki imepanga kufanya operesheni ya kijeshi ya kutengeneza ukanda wa kiusalama wa zaidi ya kilomita 30 katika miji ya Tal Rifaatna Manbij ambayo Moscow pamoja na Tehran wameitaka Uturuki kutafakari upya juu ya zoezi hilo.

Putin na Ebrahim Raisi wanatarajia kuongea kuhusu mustakabali wa kukosekana kwa chakula nchini Ukraine

Uturuki imekuwa ikifanya siasa za kufungana na pande zote mbili ambapo hivi karibuni iliunga mkono jitihada za Finland na Sweden kujiunga na NATO lakini pia imekuwa ikipinga baadhi ya vikwazo kutoka kwa nchi za Magharibi vinavyoelekezwa Moscow.

Leave a Comment