
NCHI ya Uingereza imeweka rekodi mpya ya ongezeko la joto hadi kufikia kiasi cha 40.2C katika Jiji la London kufikia majira ya saa 12:50 BST, ikivunja rekodi ya 39.1C iliyowekwa katika Mji wa Charlwood, Surrey.
Mnamo siku ya Jumanne joto linatarajiwa kuongezeka hadi kufikia nyuzi joto 42. Nchi ya Scotland pia inatarajiwa kuvunja rekodi yake ya joto ya 32.9C

Jumla ya watu watano (5) wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na hali ya hewa hiyo ya joto kali kuwahi kutokea katika nchi hiyo.
Tayari Mamlaka inayohusika na masuala ya hali ya hewa imetoa tahadhari kwa wakazi wa maeneo ya katikati, Kaskazini na Kusini- Mashariki mwa Uingereza.