Kupitia Jukwaa la Mkapa Legacy 2022, Vodacom Yaelezea Mikakati Kusaidia Sekta ya Afya
Global Publishers July 17, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Vodacom Group, Mwamvita Makamba akizungumza kwenye kongamano la pili la Mkapa Legacy 2022 linalofanyika visiwani Zanzibar, wakati wa mada ya Mageuzi ya kimkakati ya Afya nchini kupitia muungano wa biashara ya afya ( Accelerating strategic health transformation in Tanzania through business coalition for health) ambapo Vodacom Tanzania Foundation wanatoa huduma ya afya kupitia program za m-mama, fistula inatibika, wazazi nipendeni, washable sanitary pads pia wamedhamini kongamano hilo. Kulia ni Sarah Maongezi kutoka Taasisi ya Agakhan health services na muongoza mjadala Dkt. Faustine Ndugulile. Makamu wa kwanza wa Rais Serikali ya mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud akizungumza kwenye kongamano la pili la Benjamin Mkapa Foundation ( Mkapa Legacy 2022) liliofanyika kisiwani Zanzibar. Waziri wa Afya , Ummy Mwalimu akizungumza kwenye kongamano la pili la Mkapa Legacy 2022 liliofanyika kisiwani Zanzibar.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benjamin Mkapa Foundation, Dkt. Ellen Senkoro akizungumza kwenye kongamano la pili la Mkapa Legacy 2022.
Mama Anna Mkapa akiwa na mama Shadya Karume wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa inaendelea kwenye kongamano la pili la Mkapa Legacy 2022.