
NCHI ya Urusi imepanga kufanya mazoezi ya kivita katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo ikiwa na lengo la kuwaonesha wapinzani wake ambao ni mataifa ya magharibi kwamba licha ya kuwa inaendelea kushiriki katika vita yenye gharama kubwa nchini Ukraine lakini bado ina uwezo wa kuilinda mipaka yake.
Mazoezi hayo yanatarajiwa kuanza Agosti 30, 2022 kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani wan chi hiyo.
Taarifa zinadai Urusi haijawahi kusitisha mazoezi ya kijeshi na imesisitizwa kuwa katika mazoezi hayo majeshi yatapewa kila aina ya mahitaji ikiwemo watu, fedha, silaha pamoja na zana za kivita.
“Tunawaonesha kwamba ni sehemu fulani tu ya Jeshi la nchi ambayo inahusika na operesheni maalum nchini Ukraine, idadi ambayo inatosha kabisa kukamilisha majukumu waliyopewa na Mkuu wa Majeshi wa nchi hii.” Imebainisha taarifa hiyo.

Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikipotosha kwa kutoa taarifa isiyokuwa sahihi juu ya operesheni hiyo vikidai kuwa Urusi inakusanya wanajeshi wapya kwa ajili ya kuongeza nguvu katika jeshi la nchi hiyo.
Ingawa licha ya hasara kubwa inayopatikana katika vita dhidi ya Ukraibe Rais wa Urusi Vladimir Putin hana mpango wa wa kuagiza majeshi ya ziada ili kuongeza nguvu kwenye majeshi ya nchi hiyo.