×

Arsenal Yamtangaza Odegaard Kuwa Nahodha Mpya, Arithi Mikoba ya Xhaka

Nahodha Mpya wa Arsenal Martin Odegaard

KLABU ya Arsenal imemtangaza rasmi Martin Odegaard kama Nahodha mpya kuelekea msimu mpya wa 2022/2023.

 

Arsenal ilimsajili mchezaji huyo kutoka timu ya Real Madrid kwa mkopo kabla ya kukamilisha dili la kumsajili moja kwa moja kwa ada ya Paundi milioni 30 kufuatia kufanya vizuri ndani ya kikosi hicho cha washika mtutu wa London.

Odegaard kabla ya kujiunga na Arsenal alikuwa ndani ya kikosi cha Real Madrid

Kabla ya Odegaard kitambaa cha unahodha kilikuwa kikivaliwa na Granit Xhaka huku akisaidiwa mara kadhaa na kinda wa timu hiyo Bukayo Saka.

Odegaard anachukua kitambaa kutoka kwa Granit Xhaka

Tayari Arsenal ipo katika maandalizi ya msimu mpya huku ikitarajiwa kufungua pazia la Ligi Kuu nchini Uingereza ambapo inatarajiwa kucheza dhidi ya Crystal Palace siku ya Ijumaa ya Agosti 5, 2022.

Leave a Comment