
IKULU ya White House imeonya kuwa China inaweza kutumia matumizi ya zana za kivita ikiwemo kurusha makombora, ndege pamoja na meli za kivita karibu na eneo la Kisiwa cha Taiwan endapo tu Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi atatia mguu nchini humo.
Msemaji wa White House John Kirby amebainisha kuwa Spika Pelosi tayari ameshatua katika ardhi ya Malaysia siku ya Jumanne katika ziara yake ndani ya Bara la Asia.
Taiwan ni kisiwa kinachojitegemea lakini China inakihesabu kuwa sehemu ya nchi hiyo. Tayari Beijing imeshatahadharisha kuwepo kwa madhara makubwa endapo endapo Pelosi atatia mguu katika kisiwa hicho.

Vyombo vya habari vya Taiwan pamoja na Marekani vimeripoti kuwa Pelosi atazulu katika eneo la Taipei Jumanne usiku, ingawa hadi sasa hakuna taarifa rasmi ambayo imeshatoka kuthibitisha hilo.
Licha yakuwa Marekani inaamini kuwa ziara hiyo ya kisiwani Taiwan siyo rasmi lakini Marekani na China imekuwa na uhusiano ambao ni rasmi lakini wenye changamoto nyingi hasa linapokuja suala la Marekani kukitambua Kisiwa cha Taiwan kama kisiwa huru ambacho hakitakiw kuwa chini ya utawala wa china.