×

Rais Zelensky Asema Vita Vilianza na Crimea na Lazima Viishe kwa Ukombozi Wake

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky

RAIS wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema vita kati ya Urusi na nchi yake vilianzia katika ukamatwaji wa Jimbo la Crimea kwa majeshi ya Urusi kwahiyo oparesheni ya kulirudisha jimbo hilo ni kipaumbele namba moja kuelekea kutafuta uhuru kamili wa nchi hiyo.

Mlipuko umeonekana maeneo ya Crimea

Katika mlipuko huo mtu mmoja amepoteza maisha, mlipuko huo ulitokea siku ya Jumanne lakin Rais wa Ukraine hakuzungumzia mlipuko huo katika mazungumzo yake bali alisema kuwa Crimea ni sehemu ya nchi yake na kwamba hajawahi kufikiria kuiacha.

 

Wizara ya ulinzi imesema kuwa risasi zililipuka kwenye kambi hiyo, lakini Ukraine imekanusha kwamba haikuhusika na mlipuko huo.

 

Zelensky amesema Crimea lazima ikombolewe na kuwa chini ya milki ya Ukraine

Pia Maafisa wa Ukraine wamesema kuwa watu 11 wameuawa katika mashambulizi ya usiku ya Urusi Katika eneo la Dnipropetrovsky na mtu mwingine mmoja huko katika eneo la Zaporizhia kusini.

 

Crimea inatambulika kimataifa kama sehemu ya Ukraine, lakini rasi ya Bahari nyeusi ilitawaliwa na Urusi tangu mwaka 2014 baada ya kura ya maoni ambayo jumuiya ya umoja wa mataifa inaiona kuwa haramu Waukraine wanaona kuwa mgogoro wa eneo hili kuwa ni mwanzo wa vita vingine na Urusi.

Leave a Comment