×

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Haitamtaja Mshindi wa Uchaguzi wa Urais Leo

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Wafula Chebukati, akiongea jambo

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) haitamtaja mshindi wa uchaguzi wa Urais leo.

Haya ni kulingana na mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati, ambaye pia alikiri kwamba vyombo vya habari vimeanza kujumlisha ura hizo kwa kutumia Fomu 34A zilizopo.

Katika kikao na wanahabari Jumatano alasiri, mkuu huyo wa IEBC pia alikariri kuwa matokeo yatakayotangazwa katika vituo vya kupigia kura yatakuwa ya mwisho. Bw Chebukati alibainisha kuwa IEBC bado haijapokea nakala halisi za Fomu 34A au 34B.

“Ukusanyaji wa matokeo kutoka maeneo bunge 290 unaendelea na wasimamizi wa uchaguzi watatoa fomu 34B baadaye,” alisema.

“Tunawahimiza wagombea ambao wameshindwa katika uchaguzi wakubali.”

Leave a Comment