×

Mama Shamte Apokea Msaada Kutoka kwa Mfanyabiashara Maarufu PCK, Wadau Wengine Pia Waguswa

Salma Shamte akikabidhiwa pesa kiasi cha Shilingi Laki mbili 200,000/= alizopokea kutoka kwa mfanyabiashara maarufu PCK

SALMA Shamte, Mjane kutoka eneo la Mbagala- Mbande jijini Dar es Salaam ambaye hivi karibuni alihojiwa katika kipindi cha Mapito kinachorushwa na Studio za Global TV na 255 Global Radio hatimaye amepokea msaada wa kiasi cha Shilingi 200,000/= kutoka kwa mdau wa kipindi cha Mapito, mfanyabiashara maarufu, Patrick Christopher maarufu kama PCK.

 

Mbali na msaada huo wa PCK Salma Shmate pia amepokea msaada wa pesa ya ada kiasi cha Shilingi 16,5000/= ambayo imelipwa moja kwa moja kwa shule ya Sekondari ya Ashira Girls iliyopo mkoani Kilimanjaro ambako anasoma mtoto wa mama huyo.

Salma Shamte, Mama Mjane

Aidha amepewa kiasi kingine cha shilingi 55,000/= kama pesa ya matumizi yam toto wake akiwa shuleni.

 

Kiasi cha shilingi Laki mbili (200,000/=) alichopewa Salma Shamte na mfanyabiashara PCK ni kwa ajili ya mtaji wa kufanya biashara na kuongeza kipato chake binafsi.

PCK, Mfanyabiashara Maarufu

Ikumbukwe kuwa kupitia kipindi cha Mapito kinachorushwa na Global TV na Global Radio, Salma Shamte ambaye anafahamika kwa jina la Mama Shamte alisimulia jinsi alivyodhulumiwa mirathi ya marehemu mume wake na kumuacha akihangaika na ugumu wa Maisha.

Leave a Comment