×

Sistinho: Makocha wa SWPL Waangalie Vipaji Kwenye Mashindano ya CECAFA CLQ

Sistinho

MCHAMBUZI wa soka kupitia vipindi vya michezo vya Global tv online na+255 Global Radio, Sistinho amesema makocha wa timu za ligi kuu wanawake nchini Tanzania (SWPL) wahudhurie michuano ya kuwania kufuzu ligi ya mabingwa Afrika kwa wanawake ambayo inaendelea nchini kwenye uwanja wa Azam Complex kujionea vipaji mbalimbali wachezaji ambao wanaweza kuwasajili kwenye timu zao.

Mashindano ya CECAFA kwa soka la wanawake yanaendelea nchini

“Michuano hii ni platform nzuri kwa makocha wa timu za ligi yetu kufanya scouting ya wachezaji kwani wanaweza kuwaona kwa ukaribu zaidi na kwa mara nyingi ili kujidhirihisha kabla ya kuwasajili njia ambayo naamini ni nzuri kuliko hii ya kuletewa na mawakala baada ya kutumiwa video za mechi” alisema Sistinho.

 

Michuano hiyo iliyoanza Jumatatu ambapo wawakilishi wa Tanzania bara, Simba Queens waliwafunga GRFC ya Burundi mabao 6-0, itaendelea kesho tena kwa mzunguko wa pili wa makundi

Leave a Comment