Mkurugenzi wa Mawasiliano Coca-Cola Kwanza Salum Nassor akimkabidhi meza hizo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe kwa niaba ya wafanyabiashara hao.
Dar es Salaam 18 Agosti 2022 Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola Kwanza leo imekabidhi meza za kufanyia biashara kwa wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Wamachinga wanaofanyia biashara zao katika maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam.
Makabidhiano hayo yamefanyika na Mkurugenzi wa Mawasiliano Coca-Cola Kwanza Salum Nassor na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe.
Akizungumza mara baada ya kupokea meza hizo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe aliwashukuru kampuni ya Coca-Cola Kwanza kwa kuweza kutambua umuhimu wa kurundisha baadhi ya faida yake kwa jamii.
Wote ni mashaidi kuwa kampuni ya Coca-Cola imekuwa ni mdau mkubwa wa maendeleo kwa sisi wilaya ya Kinondoni. ‘Coca-Cola walitutengenezea soko la wamachinga pale Coco beach na sasa leo wamekuja kutukabidhi meza hizi kwa ajili ya kufanyia biashara zetu. Nawapongeza sana na nawaomba waendelee na jitihada kama hizi kwa zinagusa jamii yetu moja kwa moja.
Gondwe pia aliwapongeza wamachinga kwa kukubali kuacha kufanyia biashara holela holela na kwenda rasmi maeneo yao waliotengewa. ‘Mkiwa mkifanya biashara maeneo yanayotambulika kama hapa ni rahisi kupata misaada mbali mbali kwani hata kupatikana kwenu ni rahisi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Coca-Cola kwanza Salum Nassor alisema kuwa kampuni ya Coca-Cola Kwanza ni mdau mkubwa wa maendeleo na kwamba wataendelea kusaidia jamii kwa manufaa ya kukuza uchumi wa nchi.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wamachinga wa Mwenge, Mwenyekiti wa Wamachingwa kwa wilaya ya Kinondoni Abdallah Mwakilima alisema kuwa Coca-Cola kwanza wamefanya jambo njema kwani kwa sasa watakuwa na meza za kufanyia biashara na kuachana na utaratibu wa kufanya biashara kwa kumwanga bidhaa chini.
‘Tunawapongeza sana Coca-Cola Kwanza kwani kwa sasa tutakuwa na uwezo wa kufanya biashara kwa Uhuru zaidi kwa meza hizi zitasaidia bidhaa zetu kubakia kwenye ubora na usafi” alimaliza kusema Abdallah.