×

Hawa ni Viungo Ishirini Watakaolipwa Mkwanja Mrefu kama Casemiro Akitua Man United

Casemiro anatarajiwa kuingia kwenye orodha ya viungo wanaovuta mkwanja mrefu zaidi kwa wiki Duniani

KATIKA harakati za Manchester united kukamilisha dili la kiungo mkata umeme wa kibrazili ‘Casemiro’, timu hiyo inajiandaa kumlipa mchezaji huyo kiasi kikubwa cha mshahara ili kumshawishi kujiunga na wakali hao wa jiji la Manchester.

 

United wamejipanga kumlipa mchezaji huyo kiasi cha Euro 350,000 sawa na zaidi ya Shilingi Milioni 822 kwa wiki na kumfanya kuwa ni miongoni mwa viungo watano wanaolipwa pesa nyingi zaidi duniani.

Casemiro anatarajiwa kujiunga na Manchester United hivi karibuni

Casemiro ataingia kwenye orodha hii iwapo dili lake na klabu ya Manchester United litakamilika.

Hii ndiyo orodha ya viungo ishirini watakaokuwa wakilipwa mkwanja mrefu zaidi duniani:

    1. Frenkie De Jong | Barcelona | Euro 472, 952 kwa wiki.
    2. Kevin De Bruyne | Man City | Euro 400,000 kwa wiki.
    3. Sergio Busquets | Barcelona | Euro 356,701 kwa wiki.
    4. Toni Kroos | Real Madrid | Euro 355,728 kwa wiki.
    5. Casemiro | Manchester United | Euro 350,000 kwa wiki (Iwapo dili likikamilika).
    6. Luka Modric | Real Madrid | Euro 319,247 kwa wiki.
    7. Joshua Kimmich | Bayern Munich | Euro 316,166 kwa wiki.
    8. Leon Goretzka | Bayern Munich | Euro 291,846 kwa wiki.
    9. N’Golo Kante | Chelsea | Euro 289,423 kwa wiki.
    10. Koke | Atletico Madrid | Euro 259,419 kwa wiki.
    11. Miralem Pjanic | Barcelona | Euro 253,257 kwa wiki.
    12. Bruno Fernandes | Manchester United | Euro 240,000 kwa wiki.
    13. Marco Verratti | Paris Saint-Germain | Euro 233,477 kwa wiki.
    14. Rodri | Man City | Euro 220,000 kwa wiki.
    15. Franck Kessie | Barcelona | Euro 219,533 kwa wiki.
    16. Ivan Rakitic | Sevilla | Euro 214,020 kwa wiki.
    17. Marcel Sabitzer | Bayern Munich | Euro 202,671 kwa wiki.
    18. Thomas Partey | Arsenal | Euro 200,000 kwa wiki.
    19. Thiago Alcantara | Liverpool | Euro 200,000 kwa wiki.
    20. Tanguy Ndombele | Tottenham Hotspur | Euro 200,000 kwa wiki.

Leave a Comment