×

Tuchel Ajitetea Baada ya Kichapo cha 3-0 Kutoka kwa Leeds

Thomas Tuchel

BAADA ya Chelsea kupoteza kwenye mchezo wa mzunguko wa tatu ligi kuu Uingereza wakiwa ugenini dhidi ya Leeds United, Thomas Tuchel alizungumza baada ya mechi hiyo na kutaja sababu zilizopelekea wao kupoteza mchezo huo.

 

Tuchel alitupia lawama kukosekana kwa ndege ya kusafiria  kuelekea huko katika uwanja wa Allan Road nyumbani kwa Leeds United. Tuchel alisema walisafiri kwa kutumia basi jambo lililosababisha kufika wakiwa wamechoka na kusema jambo hilo lilikuwa mwanzo wa shida zilizowapelekea kupoteza mchezo wao huo.

 

Aliongezea kwa kusema kuwa walipoteza mchezo wa jana ndani ya dakika 20 za mwanzo za mchezo kwa kushindwa kutumia nafasi walizotengeneza licha ya kuutawala mchezo huo na kuwa bora Zaidi ya wapinzani wao.

Chelsea imefungwa bao 3-0 dhidi ya Leeds United

Bao la kwanza la Leeds lilifungwa na Brenden Aaronson baada ya uzembe wa mlinda mlango wa Chelsea Eduard Mendy, bao lililofungua pazia la kichapo kwa Chelsea katika mechi iliyoisha kwa kushuhudia beki kitasa wa timu hiyo Kalidou Koulibaly akitolewa kwa kadi ya nyekundu.

 

 

Imeandikwa: Abdallah Kaputi kwa msaada wa mitandao.

 

 

Leave a Comment