×

Kiungo wa Uholanzi Georginio Wiljnaldum Avunjika Mguu Wakati wa Mazoezi,Klabu yake Yathibitisha

Kiungo wa Uholanzi Georginio Wiljnaldum

KLABU ya As Roma ya Italia imethibitisha kuwa kiungo wake mpya Georginio Wiljnaldum amevunjika mguu wakati akifanya mazoezi na timu yake ya taifa.

 

Wijnaldum ambaye amejiunga na As Roma kwa mkopo akitokea kwenye klabu ya PSG. Katika ripoti iliyotolewa na klbu yake hiyo mpya ilisema Wijlnaldum katika vipimo vilivyofanyika vilionyesha kuwa mchezaji huyo amevunjika mfupa uitwao tibia katika mguu wake wa kulia.

Georginio Wiljnaldum alipojiunga na Roma Mwezi huu kwa mkopo.

Klabu ya Roma haijaweka wazi uwa kiungo huyo atakaa nje kwa muda gani. Jeraha hilo linaleta wasiwasi kwa kiungo huyo Mholanzi kama ataweza kushiriki mashindano ya kombe la dunia yanayotarajiwa kufanyika nchini Qatar November mwaka huu.

 

Kiungo huyo ameshinda vikombe tofauti tofauti 86 katika ngazi ya taifa na kufanikiwa kufunga mabao 26 mpaka sasa. Kiungo huyo pia alihudumu katika klabu ya Liverpool ya Uingereza aliyoachana nayo msimu wa 2020/21.

 

Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao

Leave a Comment