
MSANII wa Bongo Fleva Babalevo, leo asubuhi kupitia ukurasa wake wa Instagram amemsifia msanii mwenzake Chege Chigunda kwa kufungua milango ya mziki mkoani Kigoma.
Siku ya leo mapema asubuhi Baba Levo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika akimsifia msanii mwenzake Chege Chigunda kuwa alipambana sana kufungua milango ya muziki mkoani humo akisema kuwa kabla ya hapo Kigoma ilikuwa nyuma kimziki kupitia ukurasa wake wa Instagram Baba Levo ameandika hivi.
“Kama Kigoma haitokupa heshima ya kufungua muziki acha mi nikupe mapema kaka yangu. Kigoma tulikuwa nyuma sana ulipambana sana….!!!

Ujumbe ndivyo unavyosomeka kupitia ukurasa wa Instagram wa @Officialbabalevo ambaye anamsifia msanii mwenzake huyo ambapo wawili hao wote wanatokea mkoani humo, kwa sasa baba Levo yupo chini ya lebo ya wcb inayoongozwa na msanii Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz.